Jul 29, 2013

MSHIRIKI WA TANZANIA (NANDO ) ATIMULIWA BIG BROTHER BAADA YA KUGOMBANA NA MSHIRIKI MWENZAKE


Mshiriki wa Tanzania katika shindano la bba, Nando  ametimuliwa  katika  shindano hilo baada  ya  kugombana  na  mshiriki  mwenzake  Elikem wa Ghana  siku  ya  ijuumaa  ya  tarehe 26/7/2013...
Mara tu baada ya Sulu na Annabel kutolewa kwa kura za watazamaji, Big Brother aliwaita washiriki pamoja katika kikao cha dharura kufuatia ugomvi uliotokea kati ya Nando na Elikem.

Itakumbukwa kwamba siku ya ijumaa ilitokea hali ya kutoelewana kati ya Nando na Elikem. Wawili hawa walitukanana sana na kutishiana mno. Ugomvi huo ulianzishwa na Nando.

Kwa mujibu wa sheria za Big Brother mwaka huu, kuanzisha ugomvi ni kosa ambalo hupelekea kupata 'strike' ama onyo.

3 strike rule ni mtindo unaotumika msimu huu. Kwa mujibu wa Big brother, yeyote atakaye fanya makosa matatu makubwa na kupewa maonyo matatu basi moja kwa moja anatakiwa atimuliwe..

Sheria hiyo imetumika kumtimua Nando kwa sababu 1. Alianzisha ugomvi siku ya Ijumaa, 2. Alishiriki ugomvi na Elikem na 3. Alitishia maisha, "I feel like stabbing him. A nigga like that deserves to die"...

Katika kipindi cha wiki 9 za ushiriki wake katika jumba hilo, Nando amekutwa na misuko suko kadhaa ikiwemo kuwahi kukutwa na kisu katika Party ya Channel O pia kukutwa na mkasi chini ya kitanda kitu ambacho ni kinyume cha sheria za big brother.

Kutokana na ugomvi huo Elikem alipata strike moja.

Big brother alimtaka Nando aondoke katika jumba lake hilo na kutumia fursa hiyo kuwataka washiriki wengine waishi kama watu wazima.

No comments:

Post a Comment