Jul 25, 2013

Nywele za Beyonce zang'ang'ania kwenye feni wakati wa show ya Mrs Carter World Tour

Star kutoka Hollywood, Beyonce (31) alibaki akiwa amekaa kwenye stage huku akiendelea kuimba licha ya nywele zake kujiviringisha kwenye feni lililokuwa juu ya stage alipokuwa aki-perform (Mrs Carter World Tour) July,22 Montreal, Canada. Janga hilo lilimkuta alipokuwa akiimba wimbo wake "Hello", ndipo wasaidizi wake pamoja na baunsa walisogea kumsaidia ambapo walifanikiwa kumtoa baada ya kuzikata na mkasi. 

Licha ya tukio hilo kumtokea Beyonce aliandika utani juu ya kilichomtokea kupitia mtandao wa Instagram.
"Gravity cant begiiiiiiiin to pull me out of the fan again. I felt my hair was yankiiiiiiiin, From the fan that's always hatiiiiiiiin. Virgin Remy [and] Malaysiiiiiiaaaaaan haaaaaaaaa!! I got snatched "2 snaps." Goodnight all, B,"

No comments:

Post a Comment