Jul 20, 2013

MSANII MR. BOMBA ALIYETAMBA SANA KUPITIA I.T.V, AFARIKI DUNIA



Msanii wa zamani wa Kundi la Kaole Sanaa. Mr Bomba amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu na kansa ya uvimbe wa kwenye ini. Msiba utakuwa Buguruni Malapa jijini Dar es salaam nyumbani kwa marehemu alipokuwa akiishi. Mwili utaagwa siku ya Jumatatu nyumbani kwake Buguruni na kusafirishwa kijijini kwao Mpwapwa Dodoma siku hiyo ya Jumatatu kwa mazishi. 

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALAPEMA PEPONI....AMEN!

No comments:

Post a Comment