Aug 24, 2013

Baada ya Ney wa Mitego kumchana, Madam Rita ampa big up na kumkaribisha ku-perform kwenye fainali za BSS


Madam Rita: Usiruhusu mtu akuamulie maisha yako!

Kupitia U Heard na Gossip Cop 

Friday, August 23, 2013 madam Rita aliongea juu ya tetesi kuwa yupo katika mipango ya kumfungulia mashtaka Ney na kumdai amlipe shilingi millioni 500 pamoja na ku-record album nzima kwa kumsafisha jina lake baada ya kumchafulia.



Madam Rita: nani amesema hivyo, sio kweli na wala sina mda huo na sidhani hata kama ningefanya hivyo anaweza akanilipa,kwahiyo i don't have time kwa vitu ambavyo havina faida na mimi, ingekuwa anazo na uwezo huo anao labda  ningefanya hivyo kwasababu time is money, kwahiyo muda wangu kwenda kushtakiana kwa vitu ambavyo haviwezi kunifikisha popote , sina mda huo na sijafanya hivyo kwanza nashangaa nani amesema hivyo, sina mda huo sijaenda polisi , sina hata, hata simjui, hata simfikirii yaani.

Gossip Cop: aaaaaah hivi lile songi umelisikiliza Ney wa mitego alivyokuchana .

Madam Rita: huo wimbo naufaham hata kabla hajarecord

Gossip Cop: Duuh madam we nomaaa, ehe!! ilikuaje kuaje ukaijua kabla haijatoka??

Madam Rita: nipo kwenye industry ya entertainment remember? kuna mtu ambae hanijui mimi hapa Tanzania hii

Gossip: na kweli, lakini Madam Rita ile samansi kwa Ney alipelekewa lini vile, naskia alikataa kuipokea??

Madam Rita: ha ha hahaa, nimeshakwambia sina muda wa vitu ambavyo sina faida navyo, kwanza hiyo kwenda kufanya ni gharama pia ni muda, kwahiyo muda kwangu ni very very important, angekuwa anaweza kuwa na hizo hela ningeacha vitu vingine nikaifanyia kazi, lakini  hawezi kunilipa na uwezo huo hana, kwahiyo amejipatia fursa ya kujipandisha, labda kutumia kuandika hivyo na kuimba hiyo nyimbo anaweza kubadilisha maisha yake, yote kheri, ameona furasa atumie kuwaongelewa watu hivyo labda itaweza kumsogeza mbele, na kama haita msogeza mbele mi nitapata thawabu.

Gossip: na kweli, ila Ney wa mitego hivi alifaham faham vipi kwamba washindi wa BSS hawapatagi mitonyo yao ya millioni 50

Madam Rita: Sikiliza mimi hata huu mda nilioongelea hicho kitu ni wast of time, kwahiyo mi naomba tumalizie hapo kwasabau he is not worth my time, hata mimi kumtaja jina lake mimi nakua nimemuongezea nanii, kwahiyo basically nimeongea hivyo ulivyoniuliza na staki kupoteza muda wangu kumuongelea mtu ambae hana faida na mimi 

Gossip: Madam samahani lakini hivi anaitwa nani yule jamaa?

Madam Rita  mimi simjui hahahahahahaaaaaaaa

Gossip: nani wa mitego??

Madam Rita: hahahaaaaaa simjui hahahaaaa kusema ukweli mimi simjui nikwambie ukweli, simjui mtu anaitwa nini sijui nini  ndo hivyo unaona, lakini ukizingatia sasa nimeshamjua, amefanya na mimi nimjue pia sooo yaaah he is creative, big up to him big up, he is creative young man.

Gossip: Unaonaje akija ku-perform kwenye fainali za BSS


Madam Rita: aje ata-perform, tena a-perform wimbo huo huo, kwenye fainali nimesha m-book ye ndio ata-perform wa kwanza kabisa, unaona eeeh, yaani anakaribishwa ku-perform kabisa, sisi tupo hapa kubadilisha maisha ya vijana.

Sikiliza hapa...

No comments:

Post a Comment